SHARE OUR BLOG

NEW SADATH BOUTIQUE 2 & SADATH BOUTIQUE 1

MICHELLE FASHIONS

Wednesday, August 17, 2016

TIMU YA JAMIIFORUMS YAPATA AJALI MAENEO YA MBAONI-URAMBO

🔵TAARIFA​

Tunasikitika kutangaza kutokea kwa ajali ya timu (2) ya wana Jamii Media, waliopo kwenye safari za mradi wa TUSHIRIKISHANE (JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane") iliyotokea hapo jana saa 5 asubuhi, maeneo ya Mbaoni - Urambo (Tabora). Timu hiyo ilikuwa na Meneja Uendeshaji na Mikakati wa Jamii Media, Bi Asha D. Abinallah na Afisa Miradi Bw. Ericus Kimasha.

Timu hiyo ilikuwa ikielekea Kigoma mjini ili kukutana na wenzao ambako walikuwa na ratiba Warsha, kwa ajili ya kuendeleza shughuli za Mradi wa TUSHIRIKISHANE mara baada ya kumaliza shughuli zake hizo jimboni Nzega.

Kwa sasa hali zao si mbaya sana na wapo njiani kurudi Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

JamiiForums tunatoa shukrani za dhati kwa wana Urambo kwa Ushirikiano, Matibabu, Ulinzi na Usalama uliyotolewa wakati na baada ya ajali hiyo.